Uganda mwendo mdundo, yatoka sare na Zimbabwe

111
Matumaini ya kuingia hatua ya 16 bora kwa Uganda The Cranes  yameendelea kuwa makubwa baada ya kulazimisha sare ya goli 1-1 dhidi ya Zimbabwe katika mtanange wa Kombe la Mataifa Afrika AFCON uliopigwa leo Jumatano.
Uganda ambayo mchezo wa kwanza ilishinda dhidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefikisha alama 4 kwenye michezo miwili jambo ambalo linaipa nguvu ya kuingia hatua inayofuata.
Goli la Uganda The Cranes limefungwa na mshambuliaji wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi kabla ya Kham Biliat kusawazisha goli hilo dakika chake kabla ya mapumziko.
Zimbabwe wataitaji kushinda kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Congo kama wataitaji kufuzu hatua ya 16 bora ambayo mpaka sasa ni Nigeria pekee imepata nafasi hiyo.
Mchezo unaofuata leo Jumatano Misiri dhidi ya Congo.
Kundi A Msimamo
* Uganda alama 4
* Misri -3
* Zimbabwe-1
* Congo 1.

Author: Bruce Amani