Uganda yaichapa Rwanda nyumbani, ugenini

Timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Rwanda katika mchezo wa Kundi E, michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022.

Goli la kichwa la mshambuliaji Aziz Fahad Bayo anayekipiga kunako klabu ya Ashdod FC ya Israel lilitosha kutoa ushindi kwenye mechi hiyo iliyochezwa bila uwepo wa mashabiki kutokana na changamoto ya Janga la Virusi vya Covid-19.

Licha ya piga nikupiga kwenye lango la Uganda na Rwanda katika dakika 90 bado mchezo huo ukamalizika kwa kipigo kwa Amavubi ambao wamekusanya alama moja pekee wakati The Cranes wakiwa nazo 8 nafasi ya pili.

Mali ndiyo vinara wakiwa na alama 10 baada ya kuifunga Kenya bao 1-0 wakati Kenya nafasi ya tatu na alama mbili.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends