Uganda yamtimua kocha Desabre

Ni masaa 48 tu. Ni masaa 48 baada ya taifa la Uganda kuondolewa kwenye mashindano ya Afcon 2019 hatua ya 16 bora na timu ya Senegal. Kocha wa timu hiyo Sebastien Desabre ametangaza kujiuzulu kuinoa timu hiyo.
Sebastian Desabre aliteuliwa kuwa Kocha wa Uganda Disemba 2017 akichukua mikoba ya Micho aliyetimukia Orlando Pirates ya Afrika Kusini akiwa amedumu ndani ya kikosi cha The Cranes kwa miaka mitatu.
Taarifa rasmi kutoka FUFA Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda imesema “Tarehe 6 Julai 2019 Fufa ilikaa kikao na kocha Desabre kwa minajili ya kuvunja mkataba baina ya pande hizo mbili, Lengo kubwa la kusitisha kandarasi hiyo ni kwa manufaa ya kila upande (kwa maana Fufa na Desabre)” ilionyesha taarifa hiyo.
Baada ya taarifa hiyo FA imesema itatangaza Kocha wa muda atakayechukua mikoba ya Desabre kabla kocha mpya hajapatikana atakayeendelea na mipango ya karibuni ya timu ya taifa.
Kuondoka kwa Sebastian Desabre kumevumisha taarifa kuwa kocha huyo anaenda kujiunga na miamba ya soka la Afrika Al Ahly.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments