Uhamisho wa Bale kwenda China wasitishwa

44

Uhamisho wa Gareth Bale kwenda China umesitishwa baada ya Real Madrid kufutilia mbali makubaliano hayo. Sasa winga huyo ria wa Wales atabaki katika klabu hiyo ya Uhapania.

Bale, mwenye umri wa miaka 30, alitarajiwa kujiunga na klabu ya Jiangsu Suning ya Ligi Kuu ya China kwa mkataba wa miaka 3. Na angetia kibindoni pauni milioni 1 kwa wiki.

Kocha Zinedine Zidane alisema wiki iliyopita kuwa Bale anakaribia kuondoka Bernabeu. Zidane aliongeza kuwa kuondoka kwake kutakuwa “bora kwa kila mmoja”.

Bale alijiunga na Madrid kwa kitita cha pauni milioni 85 kutoka Tottenham mwaka wa 2013 katika kitita kilichoweka rekodi ya uhamisho kwa wakati huo.

Author: Bruce Amani