Uhamisho wa wachezaji: Tusker FC

308

Huku zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kung’oa nanga kwa msimu mpya wa ligi ya Kandanda chini Kenya, KPL, Mabingwa mara 11 wa ligi hiyo Tusker FC wamefanya usajili wa wachezaji wanne. Tusker inayoongozwa na kocha Robert Matano msimu uliopita haikuwa na matokeo mazuri na kwa sasa imeanza mikakati ya msimu mpya.

Wachezaji waliosajiliwa na Tusker ni Hillary Wandera kutoka Nzoia Sugar, Clyde Senaji kutoka Vihiga United, Amini Muzerwa kutoka Polisi ya Rwanda.

Vivile Tusker imemsajili aliyekuwa mchezaji bora katika ligi ya KPL msimu wa mwaka 2017, Michael Madoya. Madoya ametia saini mkataba wa miaka miwili na Tusker akitokea Zoo Kericho.

Kocha Robert Matano amesema lengo lake ni kuutwa ubingwa wa ligi ya KPL msimu ujao. “Nalenga kuwa shinda ligi ya KPL msimu ujao. Ni ndoto ya kila mchezaji kushinda taji la ligi na pamoja tutafaulu. ” Amesema Matano.

Author: Bruce Amani