Uingereza yawarudisha mashabiki viwanjani baada ya Covid-19

Serikali ya England imeruhusu mashabiki wa ugenini kuanza kuingia viwanjani katika mechi mbili za mwishoni mwa mbilinge mbilinge za Ligi Kuu kwa kila klabu nchini humo.

Mashabiki wa timu mwenyeji wametaarifiwa kuwa wataingia viwanjani katika mechi kubwa za timu zao ikiwa ni mara ya kwanza tangia kuibuka kwa janga la Covid-19 mwanzoni mwa mwaka 2020.

Kiasi cha mashabiki 500 wameruhusiwa kuingia kwenye mechi hizo mbili zitakazopigwa mwezi huu Mei kuanzia tarehe 17 na kuendelea.

Barua ya Mtendaji Mkuu wa EPL Richard Masters ilielekeza kuwa serikali imeruhusu asilimia 5 ya uwezo wa uwanja, mashabiki kuingia viwanjani.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares