Ujerumani yafuzu Kombe la Dunia kwa kuitandika Macedonia, Werner, Havertz watupia

Pamoja na kutawala mchezo kwa muda mrefu, iliwachukua timu ya taifa ya Ujerumani dakika karibia 50 kupata goli la kwanza kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 dhidi ya Macedonia Kaskazini mtanange uliochezwa Jumatatu usiku.

Bao kwanza likiwekwa kimiani kipindi cha pili na   kiungo mshambuliaji wa Chelsea Kai Havertz akimalizia pasi isiyokuwa na chembe ya uchoyo kutoka kwa Thomas Muller.
Kisha goli nyingine zikafungwa na mshambuliaji wa Chelsea Timo Werner bao mbili, kijana Jamal Musiala akiingia kambani pia.
Bila shaka utakuwa ni usiku wa kukumbwa kwa kijana Musiala ambaye mbali na kuchezea timu zote za vijana za England aliamua kubadilisha uraia na kuwa Mjerumani, akifunga bao lake la kwanza katika mechi tisa

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends