Ujerumani yashushiwa kipigo kikali cha 6 – 0 ugenini Uhispania

Winga wa klabu ya Manchester City Ferran Torres ametupia bao tatu – hattrick kwa mara ya kwanza katika taaluma yake ya soka wakati timu ya Ujerumani chini ya kocha Joachim Low imekutana na kipigo kizito cha goli 6-0 kutoka kwa Uhispania mtanange wa Ligi ya Mataifa Ulaya.

Hispania ambayo mechi iliyopita ilitoka sare, ilihitaji matokeo chanya ili kutengeneza mazingira ya kufuzu michuano hiyo hivyo ushindi huo unaifanya kujiunga na Ufaransa kutengeneza timu nne ambazo tayari zimefuzu michuano hiyo.

Katika tukio ambalo lilikuwa kama marudio ya fainali ya mwaka 2008 ya Euro, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Alvaro Morata alianzisha kampeni ya kufunga magoli kabla ya ingizo jipya ndani ya uzi wa Manchester City Torres kuandikisha rekodi ya aina yake.

Rodri ni miongoni mwa majina yaliyojitokeza kwenye ubao wa matokeo kutokana na kufunga goli moja wakati mchezo ukielekea jioni Mikel Oyarzabal aliongeza chuma cha sita.

Torres ameanza vyema kwenye klabu hata timu ya taifa amekuwa mchezaji muhimu na mzuri pia kwa kocha Alistica Cioba.

Author: Asifiwe Mbembela