United, Chelsea, Liverpool zatawala Premier League

Manchester United leo imewashushia kichapo timu ya Norwich City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa uwanja wa Old Trafford kwa kuichapa mabao 4-0.

Mabao ya United yalianza kupachikwa na mshambuliaji, Marcus Rashford aliyepachika mabao mawili alianza dakika ya 22 na bao la pili alipachika dakika ya 52 kwa mkwaju wa penalti huku la tatu likipachikwa dakika ya 53 kupitia kwa Anthony Martial na la nne likifungwa na Mason Greenwood dakika ya 78.

Ushindi huo unaifanya United ifikishe jumla ya pointi 34 ikiwa nafasi ya tano huku Norwich ikibaki na pointi zake 14 ikiwa inaburuza mkia nafasi ya 20.

Timu zote mbili zimecheza jumla ya mechi 22 za Ligi Kuu England.

Kwingineko……

Liverpool imeendeleza ubabe wake kunako EPL baada ya leo kuitandika Tottenham Hotspurs ya Jose Mourinho kwa goli 1-0 mtanange uliopigwa dimba la White Line.

Goli pekee limetiwa kimiani na Robert Firmino dakika ya 27 akimalizia pasi ya Mohammed Salah.

Chelsea 3-0 Burnley

Leicester City 1-2 Southmpton

Arsenal 1-1 Crystal Palace

Wolves 1-1 Newscastle

Kesho Jumapili

Aston Villa V Manchester City

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends