Usalama waimarishwa kuitazama Simba, Yanga Jumamosi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limejipanga vyema kuimarisha usalama katika mechi ya Watani wa Jadi baina ya Simba na Yanga katika Dimba la Benjamini Mkapa.

Mechi hiyo yenye historia lukuki, imepangwa kuchezwa Jumamosi ya Mei 8, 2021 katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni masaa ya Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mechi hiyo, Kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa amesema ni muhimu kila mzazi ambaye amepanga kuja na familia hasa watoro uwanjani kuwa makini na kutoruhusu watoto kuzagaa uwanjani na kupelekea kupotea.

Amesema kwa wale wenye nia ya kuibia kwa kukwapua vitu vya mashabiki kwa siku hiyo watadhibitiwa kikamilifu kuhakikisha, Wananchi wanaingia na kutoka uwanjani kwa amani na utulivu kwani Jeshi la Polisi liko makini.

Kamanda Mambosasa amesema kama kuna mwenye nia ovu na mchezo huo basi ahairishe mapema kwani mipango yake haitafanikiwa.

Simba yenye alama 61 inaongoza msimamo wa Ligi Kuu nchini Tanzania ikiwa imecheza michezo 25 pungufu ya ile ya timu iliyonafasi ya pili Yanga yenye alama 57 baada ya michezo 27.

Itakumbukwa mchezo wa kwanza uliopigwa dimba hilo baina ya klabu hizo, matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1, goli la Michael Sarpong na Joash Onyango.

Kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa ametoa rai kwa wazazi wanaopenda kwenda na Watoto uwanjani kuwa makini na kutoruhusu Watoto kuzagaa uwanjani na kupelelea kupotea.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares