Usiku mgumu kwa vilabu vya England

Vilabu vya Ligi ya Premier ya England huenda mpaka sasa havifurahii namna mambo yanavyokwenda katika Champions League, lakini kitu ambacho ni wazi ni kwamba kuna burudani katika michuano hiyo msimu huu. Liverpool na Tottenham Hotspur zimepoteza mechi zao Jumatano wakati Barcelona na Inter Milan zikiendelea kutamba.

Borussia Dortmund 3-0 AS Monaco

Paco Alcacer, Jacob Bruun Larsen na Marco Reus wote walishuka dimbani wakiwa katika hali nzuri na wote walitikisa nyavu katika kipindi cha pili wakati BVB ilishinda 3-0 dhidi ya Monaco.

Atletico Madrid 3-1 Club Brugge

Antoine Griezmann alifunga bao katika kila kipindi na Koke akaongeza jingine katika ya mwisho wakati Atletico Madrid iijiunga na BVB kileleni mwa Kundi lao na pointi sita kila mmoja. Arnaut Groeneveld aiifungia Club Brugge.

Tottenham Hotspur 2-4 Barcelona

Lionel Messi aifanya vitu vyake, kwa kufunga mabao mawili na kuchangia katika mengine mawili wakati Barca waliwazidi nguvu na maarifa Tottenham Hotspurs uwanjani Wembley. Ivan Rakitic na Philippe Coutinho pia walifunga, huku Harry Kane na Erik Lamela wakiwafungia wenyeji.

PSV Eindhoven 1-2 Inter Milan

Wageni hao wa Serie A walijikuta Yuma kupitia bao la Pablo Rosario, lakini Radja Nainggolan akasawazisha kabla kipindi cha mapumziko na Mauro Icardi akafunga la ushindi katika dakika ya 60 na kuiweka Inter pointi sita sawa na Barcelona kabla ya timu hizo kukutana

Napoli 1-0 Liverpool

Bao la ushindi la Lorenzo Insigne liliipa Napoli pointi tatu ilizostahiki katika siku ambayo waliwadhibiti na kuwazuia Liverpool kupiga shuti lolote kwenye lango lao.

Paris Saint-Germain 6-1 Red Star Belgrade

PSG ilipata ushindi huo mnono kupitia hat trick ya Neymar pamoja na mabao ya nyota wengine watatu Edinson Cavani, Angel Di Maria, na Kylian Mbappe. Marko Marin alifunga bao katika dakika ya 74 wakati timu yake ilikuwa nyuma kwa mabao 5-0

Lokomotiv Moscow 0-1 Schalke

Chipukizi Weston McKennie liunga bao lake la kwanza katika Champions League kupitia kichwa safi katika dakika ya 88 na kuipa Schalke ushindi huo mkubwa nchini Urusi.

Porto 1-0 Galatasaray

Moussa Marega aliunga bao pekee wakati Porto ilijiunga na Schalke kileleni mwa kuni lao na pointi nne kila mmoja.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends