Valencia wasusia mchezo watoka uwanjani kutokana na ubaguzi wa rangi

Wachezaji wa klabu ya Valencia inayoshiriki Ligi Kuu Hispania walisusia mchezo na kutoka nje ya uwanja kwenye mechi dhidi ya Cadiz iliyomalizika kwa kipigo cha goli 2-1 baada ya mchezaji mmoja wa timu hiyo kubaguliwa.

Valencia waliamua kutoka nje baada ya mchezaji wao Mouctar Diakhaby kuwaambia kuwa amesikia akitukanwa na kutolewa maneno ya kibaguzi kisha wakakubaliana kutoka uwanjani.

Wakiwa kwenye hali ya kutoelewana baina ya Mouctar na mchezaji wa Cadiz Juan Cala, Cala 31, alimtolea lugha ya kibaguzi Diakhaby.

Hata hivyo, baada ya mazungumzo na refarii, Diakhaby, 24, aliwaomba wachezaji wenzake kurudi uwanjani, walirudi na mechi kuendelea ingawa walipoteza kwa bao 2-1.

Valencia wamesema wanamuunga mkono mchezaji wao kwa kitendo cha kutoka uwanjani.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares