Valencia yaichapa Barcelona

Kocha mpya ndani ya kikosi cha Barcelona Quique Setien amepokea kichapo cha kwanza cha La Liga leo Jumamosi baada ya kuchapwa goli 2-0 dhidi ya Valencia.

Valencia ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo ushindi kwao sio tu jambo kubwa bali limevunja rekodi mbaya ya kutoshinda mtanange wowote dhidi ya Barca tangu mwaka 2007.

Gomez alikuwa mwiba wa mchezo aliyeandikisha ushindi wa leo kwa kufunga goli mbili dakika ya 43 na 77 kabla ya hapo awali kukosa penati iliyookolewa na Ter Stegen.

Utawala wa Setien ulianza na mwanzo bora kufuatia kushinda mechi mbili dhidi ya Granada na UD Ibiza kombe la Copa del Rey.

Matokeo yanaifanya Barca kuwa hati hati ya kukosa uongozi wa La Liga endepo Real Madrid ikishinda mchezo wake dhidi ya Real Valladolid.

Author: Bruce Amani