Van Gaal kusalia Uholanzi licha ya matokeo mabovu na afya kutetereka

117

Jina la kocha Louis van Gaal litaendelea kutamkwa tena kwa Waholanzi licha ya wengi wao kusema aondoke kufuatia matokeo mabovu kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 dhidi ya Norway ambao umebeba matumaini kibao.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 70, mbali na kuwa na matokeo mabaya pia hali yake kiafya bado haijaimarika ambapo leo Jumatatu Novemba 15 amefanya mazungumzo na Waandishi wa Habari akiwa kwenye viti maalumu.

“Sina utimamu wa mwili lakini akili yangu inaifanya kazi vizuri”, alisema Van Gaal kocha wa zamani wa Manchester United.

Nahodha wa timu hiyo Virgil van Dijk, alisema tukio la kocha huyo kuugua lilikuwa la kushangaza lakini sasa hali yake afadhali.

Uholanzi ilitoka chini kwa bao 2-0 na kusawazisha na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2 dhidi ya Montenegro Jumamosi ambapo sasa wamepoteza nafasi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia Qatar 2022 kabla ya mchezo wa mwisho.

Jumanne watacheza na Norway ambapo sare inaweza kuwapa nafasi hiyo.

Author: Bruce Amani