VAR yaipokonya City ushindi dhidi ya Spurs

47

Ligi Kuu ya England imeendelea leo wiki ya pili tangu utepe wa EPL kukatwa, matajiri wa Manchester City wamebanwa mbavu na Tottenham dimba la Etihad 2-2, Liverpool yatakata ugenini.

Manchester City ikiwa dimba la Etihad imeshindwa kufurukuta mbele ya wageni Tottenham Hotspurs ambapo mchezo umeenda kwa sare ya goli 2-2.

Raheem Sterling na Kun Aguero walifunga goli moja kila mmoja wakati goli za Tottenham zikifungwa na Erik Lamela, na Lucas Moura, kabla ya dakika tisini kuisha, Gabriel Jesus alifunga goli lililokataliwa na VAR.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester City kujikusanyia alama nne sawa na Tottenham baada ya timu zote kushinda mchezo wa awali.

Liverpool imeendelea kufanya vyema, ikishinda mtanange wa kwanza dhidi ya Norwich City 4-1 kisha ikashinda 5-4 kwa penati katikati ya wiki dhidi ya Chelsea na leo wameitandika Southmpton goli 2-1 ugenini.

Sadio Mane na Roberto Firmino wamehusiska kupeleka kilio kwa Soton huku goli la kifungwa na Che Adams. Katika EPL Liverpool imefikisha alama sita sawa na Arsenal.

Everton chini ya kocha Brendan Rogers imefanikiwa kupata alama tatu dhidi ya Watford katika mchezo uliopigwa Goodson Park, goli pekee la Bernard lilitoa ushindi wa Everton hawo ambao wamesajiliwa majina mengi msimu huu.

Matokeo mengine EPL.

Aston Villa 1-2 Bournemouth

Brighton 1-1 West Ham

Jumapili ni mtihani mwingine kwa Frank Lampard kucheza dimba la nyumbani kwa mara ya kwanza dhidi ya Mbweha Leicester City, mtanange mwingine utakuwa kati ya Sheffield United vs Palace.

Author: Bruce Amani