Varane, Maguire wampasua kichwa Solskjaer

Majanga, kocha amekuwa akipewa lawama za kushindwa kupata matokeo bora kutoka kwa wachezaji bora. Wakati huo huo lawama zilitolewa, majanga yanampata tena Ole Gunnar Solskjaer na kikosi chake cha Manchester United kufuatia kulazimika kumkosa beki wa kati Raphael Varane kutokana na majeruhi.

Majeruhi ya Varane yametokea akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Ufaransa wakati ilichuana na Hispania fainali ya Ligi za Mataifa siku ya Jumapili.

Nyota huyo mwenye miaka 28, ameshaanza mechi 6 tangia kusajiliwa kutokea Real Madrid mwezi Agosti.

Varane anaumia kipindi ambacho kocha Solskjaer anaendelea kukosa huduma ya beki Harry Maguire.

Taarifa za kitaalamu zinasema atakuwa nje kwa angalau wiki kadhaa, kuanzia mchezo wa Jumamosi dhidi ya Leicester City Ligi Kuu England.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends