Vilabu EPL vyakubaliana kuanza mazoezi ya pamoja na kugusana

Vilabu vya Ligi Kuu England vimekubaliana kuanza mazoezi ya pamoja kufuatia kufanya mazoezi ya makundi madogo madogo kwa takribani wiki mbili licha ya kesi za maambukizi pia kuwepo nchini humo.

Jumla ya vipimo 1,008 vya wachezaji na viongozi vimeshafanyika katika raundi tatu za awali na kubaini watu wanne wameathirika na virusi vya Corona.

Makubaliano hayo yanamaanisha kuwa wachezaji wataanza kugusana wakifanya mazoezi hata kuangushana (tackling) pia kumeruhusiwa licha ya katazo la kugusa pasipo sababu.

Watu 12 pekee wamekutwa wameathirika na virusi hivyo katika jumla ya vipimo 2,752 vilivyofanyika.

Wachezaji na viongozi watakuwa wanapimwa mara mbili, endapo mmoja wapo atakutwa na virusi vya Corona atawekwa karantini kwa siku saba za matazamio.

Alhamis ijayo, vilabu vitajadiliana juu ya kurejea kwa EPL ambapo miongoni mwa hoja zitakazojadiliwa ni pamoja na matumizi ya viwanja huru, na utaratibu wa matangazo yatakavyokuwa.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends