Utamaduni ni kitu kinachobadilika siku hadi siku. Utamaduni ambao ulikuwa mgumu kuzoeleka sasa unaonekana utakuwa ni utamaduni wa kawaida kwa vilabu na wachezaji hivi sasa.
Kucheza bila uwepo wa mashabiki inaelekea kuwa kawaida, ambapo ili wachezaji kuzoea hali hiyo imelazimika kuanza kuchezwa kwa mechi za ndani ya klabu ili kupata hali halisi kwa wachezaji.
Ligi kuu ya England imekusudia kuanza kuchezwa tena Juni 17 kwa michezo miwili viporo baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi mitatu kutokana na janga la virusi vya Corona.
Manchester United imecheza mchezo wao wakigawa timu mbili kila upande, Chelsea wamefanya hivyo katika dimba la Stamford Bridge, Wolverhampton Wanderers, Tottenham Hotspur pia imefanya hivyo pamoja na vilabu vingine vya EPL ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao.