Vilabu vya EPL vyaruhusiwa kucheza mechi za kirafiki

Vilabu vya Ligi Kuu nchini England vimepewa ruhusa ya kuanza kucheza mechi za kirafiki huku zikizingatia kanuni na taratibu mbalimbali za wataalamu wa afya.

Ruhusa hiyo inakuja katika kipindi ambacho ligi inakusudiwa kurejea tena mwezi Juni 17 bila uwepo wa mashabiki.

Jana Jumatatu vinara wa ligi kuu nchini England Liverpool walikuwa wa kwanza kufanya mazoezi ya kugawana wachezaji 11 kwa 11 kwenye dimba lao la Anfield.

Mechi za kirafiki zitachezwa bila uwepo wa mashabiki lakini inaweza ikawa katika viwanja vya mazoezi au viwanja maalumu vya mechi.

Wakati mechi za kirafiki zinaruhusiwa ni lazima mambo haya kuyazingatia kwa wachezaji na viongozi wa EPL:-

Wachezaji/timu hawatakiwi kusafiri kwa umbali mrefu baada ya mchezo, timu pekee ya Newcastle United imeruhusiwa kusafiri zaidi.

Wachezaji wote wanatakiwa kusafiri katika usafiri wao na mavazi yao.

Waamuzi rasmi hawata ruhusiwa kuchezesha mechi hizo.

Lazima viwanja na vifaa vipuliziwe dawa kabla na baada ya michezo hiyo kuhakikisha kuna usalama kwa wachezaji na viongozi wa EPL.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends