Virgil van Dijk anahitaji upasuaji wa goti

390

Beki wa Liverpool Virgil van Dijk anahitaji upasuaji wa goti lake baada ya kupata majeruhi kwenye mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya Everton mtanange wa Ligi Kuu England uliopigwa Jana Jumamosi. Beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 29 alishindwa kuendelea na mchezo baada ya faulo ya kipa Jordan Pickford ungwe ya kwanza.

Bado haifahamiki atakaa nje kwa muda gani, maana amepelekwa kwenye vipimo ili kujua ukubwa wake. Baadhi ya vyanzo vya habari vinasema Virgil anaweza asiwe sehemu ya kikosi cha Liverpool kwa msimu huu wote.

Van Dijk amekuwa mchezaji muhimu kwa Liverpool tangu aliposajiliwa mwaka 2018 akitokea Southampton kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 75.

Author: Bruce Amani