Virusi vya Corona vyatishia kusitishwa mechi za Italia

Inter milan wanategemea kucheza mchezo wa nyumbani dhidi ya Ludogorets wa Ligi ya Europa hatua ya 32 bila mashabiki kwa kuhofia kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona.

Inter ni miongoni mwa timu nne za Serie A kusitisha kuchezwa michezo ya Ligi wikendi iliyopita kutokana na hofu hiyo.

Mazungumzo yamekuwa yakiendelea kati ya klabu, viongozi wa serikali ya Italia na uongozi wa soka barani ulaya kujua hatima ya ratiba ya mchezo wa Alhamis.

Tangu kuanza kuenea kwa virusi hivyo kwenye maeneo mengine nje ya China, Italia ni nchi inayoongoza kwa idadi kubwa ya waathirika wa virusi hivyo barani ulaya ambapo sasa imefikia idadi ya wagonjwa 165, huku shule na vyuo mbalimbali vikiwa vimefungwa licha ya usafiri wa umma kuendelea kama kawaida.

Zaidi ya mashabiki 600 wa Ludogorets wanatarajiwa kusafiri kutoka Bulgaria kwa ajili ya mtanange wa Alhamis utakaopigwa dimba la San Siro mkondo wa kwanza.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini Italia siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa Taifa hilo amesema “Tutaendelea kujaribu kusitisha mikusanyiko yote inayohusisha watu wengi hata wiki lijalo(kwa maana wiki hii).

Miji miwili pekee ya Lombardy na Veneto yenye zaidi ya watu 50000 ndiyo imewazuia raia wake kutoka nje ya mipaka ya miji hiyo bila ruhusa maalumu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends