Vita wa kuongoza La Liga yanoga, Real Madrid yaiadhibu Granada

344

Magoli mawili ya Casemiro na Karim Benzema yamewapa ushindi muhimu Real Madrid dhidi ya Granada katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga na kufanana alama na vinara Atletico Madrid.

Baada ya kuwa na mwanzo mbaya wa mechi hiyo, Madrid walirudi kipindi cha pili na nguvu na kufanikiwa kupata goli hizo mbili, Casemiro alimalizia krosi ya Marco Asensio.

Benzema aliipa uhakika wa matokeo chanya dakika za mwishoni likiwa ni goli lake la nane kwenye La Liga.

Unakuwa ushindi wa sita mfululizo kwa kikosi cha kocha Zinedine Zidane katika mashindano yote, na tano mfululizo ndani ya La Liga wakitoshana alama 32 na vinara Atletico ingawa wananufaika na mechi mbili zaidi za kucheza.

Author: Bruce Amani