Waamuzi wa Tanzania Derby Simba Vs Yanga wajulikana

Kuelekea mtanange wa Ligi Kuu nchini Tanzania baina ya wenyeji Simba dhidi ya Yanga, Shirikisho la Soka Tanzania limetangaza orodha ya waamuzi wanne watakaotumika kuamua mechi hiyo itakayofanyika Jumamosi Mei 8.

Tofauti na michezo mingine ya VPL iliyopita ya karibuni, mchezo wa Simba na Yanga wa awamu hii utachezeshwa na waamuzi watatu na mmoja wa akiba jumla wanne.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili kwa watani hao kukutana ambapo ule wa raundi ya kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Novemba 7 ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imemtaja Emmanuel Mwandembwa kutoka Arusha kuwa mwamuzi wa kati.

Frank Komba wa Dar kuwa mwamuzi msaidizi namba moja.

Hamdan Said kutoka Mtwara kuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.

Na Ramadhan Kayoko kutoka Dar kuwa mwamuzi wa akiba.

Licha ya utani na ushindani uliopo kwenye mechi hiyo, bado haitabadili lolote kwenye msimamo wa Ligi kwani Simba wamecheza mechi pungufu lakini wanaizidi Yanga alama nne.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares