Wachezaji wa Brazil wapinga kuwa wenyeji wa Copa America

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Brazil wamekosoa maamuzi ya Shirikisho la Kandanda nchini humo kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano ya Copa America.
Shirikisho la Amerika Kusini Juni Mosi liliyahamisha mashindano ya Copa America kutoka kwa taifa mwenyeji Argentina mpaka Brazil kwa kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya virusi vya Corona.
Likiwa ni pigo la pili kufuatia, taifa la Colombia lililokuwa mwenyeji mwenza wa Argentina lilijitoa tangu awali kwa sababu ya kukosa utulivu ndani ya taifa lao.
“Kwa sababu yoyote ile, kiutu, kitalaamu, hatujaridhishwa na fainali za Copa America kufanyika nchini kwetu”. Kupitia barua rasmi ya wachezaji kwenda shirikisho la soka la Conmebol.
Vyombo vya Habari mbalimbali nchini Brazil vimeripoti kuwa wachezaji hawakufurahishwa lakini hawatagomea mashindano hayo.
Ujumbe wa wachezaji ulitolewa muda mfupi baada ya mechi dhidi ya Paraguay ambayo walishinda bao 2-0 ya kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares