Wachezaji ligi ya Ujerumani wakiuka kanuni za kutokumbatiana, DFL yawatadharisha

185

Wachezaji wa ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga wamekumbushwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na virusi vya Corona wawapo uwanjani.

Tahadhari hiyo inakuja baada ya wachezaji wa Hertha Berlin kukiuka utaratibu huo katika ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Hoffenheim.

DFL ilishasema tangu wikiendi iliyopita kuwa wachezaji wa Hertha Berlin hawata adhibiwa kutokana na ushangilia wao ndio maana wametoa onyo hilo.

“Kuna utaratibu maalumu ambao inatakiwa kila mmoja afwate”. Yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bundesliga Kimataifa Robert Klein

“Vilabu vimekuwa vikifanya kazi kubwa sana, kila siku wanaongea na wachezaji juu ya kuchukua tahadhari na vitu gani vya kufanya na visivyo vya kufanya tunajua itakuwa vigumu mechi za mwanzoni lakini tutakavyokuwa itakuwa rahisi” aliongeza Klein

Kurudi kwa ligi na kucheza raundi ya kwanza salama ni mafanikio makubwa sana kwao, licha ya changamoto ya baadhi ya viwanja nje ya uwanja mashabiki kujitokeza kwa wingi lakini bado ni mafanikio mazuri.

Klein amesema kwa sababu ligi kubwa barani Ulaya hazijaanza zaidi ya Bundesliga macho yote yapo Ujerumani, hivyo wako makini kuangalia ubora wa kandanda, hata hivyo Klein amesema ligi ilikuwa inatazwa zaidi siku ya Jumamosi katika nchi ya Afrika Kusini, Colombia, Ghana na South Africa, Colombia and Ghana.

Author: Bruce Amani