Wachezaji, marefarii kuendelea kupiga magoti kupinga ubaguzi wa rangi EPL

332

Wachezaji wote kutoka kwenye klabu zote 20 za Ligi Kuu England wataendelea kupiga magoti kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ikiwa ni ishara ya kuungana kwa pamoja kupinga vitendo vyovyote vinavyoashiria ubaguzi wa rangi.

Pamoja na hayo, katika jezi za wachezaji na maofisa kutakuwa na maandishi yanayopinga ubaguzi wa rangi, mechi ya kwanza ya Ligi itachezwa baina ya wageni Brentford dhidi ya Arsenal Ijumaa Agosti 13.
Itakumbukwa mwezi wa pili klabu ya Brentford ilitangaza kuwa haitaendelea kupiga magoti kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna maana tena ya kupiga magoti.
Wachezaji walianza kupiga magoti Juni 2020 baada ya kukithiri kwa vitendo vya kibaguzi kwa Wanamichezo kukiwa na kaulimbiu ya “Black Lives Matter”.
Mtendaji Mkuu wa EPL Richard Masters, amesema kuwa wachezaji, maofisa wataendelea kupiga magoti kuungana na wanamichezo mingine kupinga vitendo kama hivyo”.
Baada ya matokeo hasi kwa England huku kukiwa na wachezaji watatu wakifanyiwa ubaguzi wa rangi wa kimataifa wa England baada ya kukosa penati Jadon Sancho, Bukayo Saka na Marcus Rashford walikumbana na kadhia hiyo.

Author: Bruce Amani