Wachezaji na viongozi 6 wa vilabu EPL wakutwa na virusi vya Corona

Mchezaji mmoja na viongozi wawili wa Watford na kocha msaidizi wa Burnley wamegundulika kuwa wameathirika na virusi vya Corona ni kufikisha watu sita waliokutwa na Covid-19 kwenye EPL.

Wachezaji na viongozi walioathirika watajitenga kwa siku saba, hata hivyo watu wawili pia wamekutwa na dalili za Corona kutoka kwenye klabu za daraja la tatu.

Wiki hili timu zimeanza mazoezi ya makundi madogo madogo ya watu wasiozidi 10 na Ligi ya England inakusudiwa kurejea tena Juni 12 baada ya takribani miezi miwili ya kutochezwa.

Jumla ya wachezaji na viongozi 748 walipimwa kutoka kwenye vilabu 19 mwanzoni mwa wiki hili ambapo klabu ya Norwich City imefanya vipimo vyake jana Jumanne.

Watford imethibitisha idadi ya waathirika licha ya majina yao kutowekwa wazi kutokana na taarifa hizo kuwa ni faragha, hata Burnley pia imethibitisha muathirika wa virusi vya Corona ambaye ni kocha msaidizi Ian Woan.

Mechi 92 zimesalia kutamatisha ligi kuu ya England

Author: Bruce Amani