Wachezaji wa kandanda la England kuanza mazoezi Jumanne katika makundi ya watu 10

Vilabu vya Ligi Kuu nchini England vimekubaliana rasmi kuanza mazoezi katika idadi ndogo ya wachezaji kuanzia kesho Jumanne kwa ajili ya kutoa nafasi ya kurejea kwa kandanda nchini humo.

Katika kura iliyopita kwa kishindo, ambayo imefanyika leo Jumatatu mwafaka umefikiwa wa mazoezi kuanza katika makundi madogo ya wachezaji 10.

Wachezaji wameambiwa lazima wazingatie maagizo yaliyokuwa yametolewa na wataalamu wa afya kama kukaa angalau mita moja, lakini pia kugusana au kusalimiana kumepingwa vikali.

Kama tulivyosema afya za wanamichezo ni kipaumbele chetu cha kwanza, kuanza mazoezi kwa hatua tena katika hali ya usalama ni jambo la heri kwetu. Imesema taarifa.

Awali taarifa ilitoka kuwa EPL ingerejea Juni 12 lakini kutokana na janga la virusi vya Corona kuonekana madhara yake kupungua kwa kiasi kikubwa huku Bundesliga kurudi huenda kukarudisha mapema kandanda nchini humo.

Wikendi iliyopita wachezaji walikuwa wanafanyiwa vipimo na klabu zao kwa nyakati tofauti.

“Ni kipindi kigumu lakini kwa mfumo wanaotaka kuuanzisha unatupa matumaini, kila mmoja atakuwa amefurahia kurudi kwa mazoezi (ya wachezaji 5 kila kundi) ni juhudi za pamoja”. Alisema Kocha mkuu wa Newcastle United Steve Bruce.

Yatakayojiri siku za usoni.

  • 19 Mei: Wachezaji wanaanza rasmi mazoezi katika makundi chini ya uangalizi maalumu.
  • 25 Mei: Siku ya mwisho ambayo inabidi tarehe za mwisho wa msimu wa ligi husika kwenye kila taifa kuwasilisha kwa Uefa
  • 1 Juni: Serikali ya England kuna uwezekano wa kutangaza urejeo wa shughuli za michezo bila uwepo wa mashabiki.
  • 12 Juni: EPL huenda ikaanza rasmi.

Author: Bruce Amani