Wakati dirisha dogo la usajili likifungwa leo Ijumaa, Yanga yafanya usajili wa mwisho kimataifa

Ni Fiston Abdulazack raia wa Burundi ambaye amemalizana na mabosi wa Klabu ya Yanga ili kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa ndani ya Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo inaelezwa kuwa amepewa dili la miaka miwili.

Walianza na Saido Ntibanzokiza kisha ikafuata Dickson Job wa Mtibwa Sugar na sasa ni zamu ya Abdulrazak.

Nyota huyo pia amewahi kucheza pia vilabu kama Klabu ya ENPPI ya Misri.

Kwenye timu ya Taifa ya Burundi amecheza jumla ya mechi 49 tangu msimu wa 2009 na ametupia mabao 19.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa lengo kubwa la kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambulia ni kufunga mabao zaid.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares