Wakala wa Haaland akutana na mabosi wa Real Madrid, Barcelona

Taarifa kutokea nchini Hispania zinaeleza kuwa Wakala wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland Mini Raiola amekutana na klabu za Real Madrid pamoja na Barcelona.

Kama haitoshi, Baba mzazi wa Haaland, Alf Inge, alikutana na wakala Raiola kisha wakafanya mazungumzo na Rais wa Barca Joan Laporta na Rais wa Real Madrid Florentino Perez.

Barcelona kwa sasa inakumbwa na madeni makubwa lakini chini ya Rais mpya wanahitaji kuwa miongoni mwa timu zinazowania ubingwa wa Ulaya, mwandishi Guielleme Balague anasema ushawishi kwa Baba mzazi unaweza ukawa na nguvu.

Real Madrid wameweka fedha tayari kwa mshambuliaji huyo ingawa mtazamo wao upo kwa winga wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe, kwa maana hiyo Haaland ni chaguo la pili.

Haaland ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni 2024, inatajwa kuwa thamani yake inafikia pauni milioni 128.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares