Wamiliki wa Man United kuyajenga na mashabiki wake

Mwenyekiti mweza wa Manchester United Joel Glazer amepanga kukutana na mashabiki wa klabu hiyo kwa mara ya kwanza katika miaka 15 aliyokaa Old Trafford kama Mmiliki Leo Ijumaa.

Familia ya Glazer ilipigiwa kilele na mashabiki wa klabu wakishinikiza kuachia madaraka baada ya wamiliki wa timu hiyo kukubali kujiunga na yaliyokuwa mashindano mapya European Super League.

Itakumbukwa maandamano yaliendelea kwa muda licha ya klabu hiyo kujiondoa kwenye uanachama wa European Super League(ESL) ambapo mchezo wa Ligi Kuu England baina ya Man United dhidi ya Liverpool Mei 2 uliahirishwa kutokana na maandamano ya mashabiki.

Baada ya tukio lile, aliomba radhi kwa mashabiki.

Kupitia kikao hicho, inaelezwa kuwa kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anatumia kuomba baadhi ya maingizo mapya kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao, miongoni mwa maeneo yanayohitaji maboresho ni eneo la ulinzi, kiungo cha chini na juu pamoja na eneo la ushambuliaji huku Jadon Sancho akielezwa kuwa anakuja kuziba eneo la winga.

Bado haiko wazi kuwa katika kikao hicho na mashabiki, Glazer atagusia kuhusu usajili au la, mashabiki watakuwa na nafasi ya kuuliza maswali.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares