Wanaharakati wataka ulimwengu ususie Michezo ya Olimpiki ya Tokyo

Muungano wa vikundi 180 vya kutetea haki za binadamu umetowa mwito wa kususia michezo ya Omlipiki itakayofanyika mwakani nchini China. Sababu kuu walioitaja ni ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya makundi ya watu walio wachache nchini humo. Muungano huo unawakilisha Watibeti, Wauighurs, Wamongolia , na wakaazi wa Hong Kong miongoni mwa makundi mengine.

Wametuma barua ya wazi kwa serikali mbalimbali ulimwenguni kususia michezo hiyo ya Olimpiki na kujiweka mbali na China inayodaiwa kukiuka haki za bindamu na kuminya upinzani. Aidha muungano huo uliwahi kuitaka Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kufanya michezo hiyo nchi nyingine isiyo China lakini madai yao yalipuuzwa. Kamati ya Olimpiki iliwajibu kwamba haijihusishi na masuala ya kisiasa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares