Wasifu wa ingizo jipya la Yanga Saidi Ntibazonkiza

Ilikuwa ni majira ya jioni ya siku ya Jumatatu siku moja baada ya mchezo uliokuwa kwenye kalenda ya Fifa kati ya Tanzania “Taifa Stars” dhidi ya Burundi ambapo baada ya mchezo ule hali ya hewa ilibadilika kabisa nchini Tanzania.
Hali ya hewa ilibadilika kufuatia mchezo ule kumalizika kwa Tanzania kuangukia pua kwa kufungwa bao moja kwa bila huku jina moja pekee likitazamwa zaidi kutokana na umaridadi wa bao lenyewe lililobadili mwelekeo wote wa masikio na macho ya Watanzania.
Pengine kama walivyosema wahenga kuwa siku ya kuja ya mwana wa Adam ni sawa na mwivi haijulikani saa wala dakika yake, ni kujiandaa siku yoyote.
Jina pekee ambalo lililobahatika kwenda na kauli ya uhenga ni lile la Saidi Ntibazonkiza ambaye siku ya pili baadae aliitwa na mabosi wa Yanga kisha wakamaliza mambo yao na kutambulishwa siku hiyo hiyo kama mchezaji huru. Ni mhenga haswa, maana ana miaka 33 ambapo Kiafrika Afrika huenda kuna miaka imekatwa lakini sio mada yangu bali wasifu wake uliotukuka.
Ntibazonkiza, ameachana na klabu ya Vital’O ametangazwa kuwa mchezaji halali wa Yanga ambao ataanza kukitumikia kikosi hicho mwezi Novemba baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa. Bao lake alifunga nje kidogo ya 18 kwa shuti kali likimuacha kipa wa Azam David Mapigano hana la kufanya.
Ntibazonkiza alianza taaluma yake katika klabu ya Vital’O mwakaa 2005 kabla ya kukimbiliana kukipiga Uholanzi, lakini mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji alisimamishwa kusakata soka la ushindani baada ya utovu wa nidhamu lakini baada ya hapo alikosa timu kabla ya kufanyia mazoezi katika klabu ya udogoni kwake.
Mwaka 2016 Novemba 18, Saidi Ntibazonkiza alicheza mchezo wake wa kwanza ndani ya Uholanzi katika klabu ya Sparta Rotterdam.
Klabu hiyo ya Uholanzi baadae ilimtoa Ntubazonkiza kwenda katika klabu ya NEC  hadi mwaka 2009, ambapo aliongeza mkataba mwingine wa mpaka 2012, hiyo ilikuwa Januari 2009.
Mwezi Februari 10, 2017 aliingia mkataba na klabu ya Kaysar Kyzylorda nchini Kazakhstan. Baada ya kuachwa na Kaysar Kyzylorda, Ntibazonkiza alirudi Burundi na kujiunga na klabu ya Vital’O. Timu ya Wananchi Yanga imekuwa miongoni mwa vilabu vya VPL ambavyo vinapigiwa chapuo la kufanya vizuri na kubeba taji la Ligi mwaka 2021/22.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares