Wasiwasi wa kusambaa maambukizi ya corona wagubika Michezo ya Olimpiki

Kuelekea michezo ya Olimîki jijini Tokyo nchini Japan, Ijumaa wiki ijayo, mmoja wa waandalizi wa michezo hiyo ameambukizwa virusi vya corona, akiwa kwenye kijiji walichofikia wachezaji mbalimbali.

Mpaka sasa kuna visa 15 vya corona ambavyo vimeripotiwa kuhusiana na maandalizi ya michezo hii na inamaanisha kuwa afisa huyo sasa atajitenga hotelini kwa siku 14.

Mwandalizi Mkuu wa Michezo hiyo, Seiko Hashimoto, amesema hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa, kwa wanamichezo wanaokuja kushiriki kwenue michezo hii.

Ripoti zinasema, afisa huyo alipowasili jijini Tokyo alipimwa na hakuwa na virusi hivyo lakini alipokwenda kwenye kijiji hicho cha wacheaji, alibainika kuwa na virusi hivyo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares