Watu 5 wakamatwa kwa ubaguzi wa rangi England

Watu watano wamekamatwa na Jeshi la Polisi England kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi mitandaoni kwa wachezaji wa taifa la England kufuatia kupoteza mechi ya fainali ya Euro 2020 kwa Italia Julai 11.

Wachezaji ambao walikutana na kadhia hiyo ni Marcus Rashford, Bukayo Saka na Jadon Sancho ambao wote walikosa penati kwenye mchezo huo wa fainali.
Mark Roberts, Mkuu wa Jeshi la Polisi alisema “Kama utabainika kuwa umefanya vitendo vya kibaguzi, hakika utajutia kufanya vitendo vya aibu kama hivyo”.
Kitengo cha Umoja wa Polisi UK pia kimesema kinaendelea kufanyia kazi ripoti mbalimbali ambazo zinahusiana na ubaguzi kwa wachezaji.
Mtu wa mwisho kukamatwa kwa tuhuma hizo alikamatwa na Jeshi la Polisi la Cheshire ambapo ana miaka 42 alikamatwa kutokea Runcorn kutokana na kuandika matusi mtandaoni yenye ubaguzi ndani yake.
Uchunguzi unaendelea ingawa ni jambo ngumu kulikomesha kwani licha ya juhudi kama hizo kunahitajika nia ya dhati ya kuhakikisha kunakuwa na uelewa wa watu wengine

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares