Waziri Mkuu Hispania asema kandanda ya La Liga linaweza kurejea tena kuanzia Juni 8

Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez amesema La Liga inaweza kuendelea kuchezwa kuanzia Juni 8 ingawa bila uwepo wa mashabiki.

Itakumbukwa Rais wa ligi ya Hispania Javier Tebas alisema ligi kuu nchini humo inaweza kuanza kuchezwa Juni 12 hivyo huenda kauli ya Waziri Mkuu ikaharakisha mchakato wa kurejesha michezo ambayo imesimama tangu Marchi 12.

Wachezaji wa La Liga wiki hii wameruhusiwa kufanya mazoezi ya makundi madogo madogo yasiyozidi watu 10.

“Hispania imefanya kila kilichotakiwa kufanyika, sasa ni wakati wa kuanza kuruhusu shunguli za kila na siku kuendelea kama ilivyokuwa kawaida”, alisema Waziri Mkuu Sanchez.

“Kuanzia Juni 8 La Liga itarejea rasmi. Mpira wa Miguu Hispania una wafuatiliaji wengi lakini haimanisha kuwa ndiyo mchezo pekee utakaorejea”. Aliongeza

Vilabu vya La Liga vimebakiza mechi 11 msimu huu, ambapo Barcelona inaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Real Madrid.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends