Wazito FC, Kisumu All Stars wapandishwa daraja KPL

Wazito FC wamerejea katika Ligi Kuu ya Kandanda Kenya – KPL pamoja na Kisumu All Stars baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza na pili mfululizo kwenye ligi ya daraja la pili ya National Super League – NSL ambayo imekamilika Jumapili.

Wakati huo huo, Nairobi Stima waliwazaba Eldoret Youth 4 – 2 na kumaliza katika nafasi ya tatu ili kuweka miadi na Posta Rangers katika matanange wa kuamua nani atapandishwa au kushushwa daraja katika KPL.

Wazito waliwagaragaza St Josephs Youth 7 – 0 katika uwanja wa Camp Toyoyo Nairobi na kubeba kombe la msimu huu la NSL baada ya ligi hiyo kushuhudia kinyanganyiro kikali. Kisumu All Stars waliwakaanga Thika United 6 – 1 na kupata kibali cha moja kwa moja cha kucheza kandanda la daraja la kwanza.

Timu hizo tatu ziliingia katika duru ya mwisho ya msimu zikitenganishwa na pointi moja tu ambapo Wazito walikuwa na faida ambayo iliwawezesha kumaliza msimu kama timu bora na pointi 81, moja mbele ya Kisumu ambao walimaliza katika nafasi ya pili

Matokeo ya mechi za mwisho za NSL

Kenya Police 2-2 Ushuru (Karuturi Grounds)

Migori Youth 2-0 Kangemi All-Stars (Awendo Stadium)

Fortune Sacco vs Modern Coast Rangers (Kianyaga Stadium)

Kibera Black Stars 1-2 Nairobi City Stars (Hope Center)

Green Commandos vs Coast Stima (Bukhungu Stadium)

Wazito 7-1 St. Joseph’s Youth (Camp Toyoyo)

Administration Police vs Bidco United (Ruaraka Grounds)

Thika United 1-7 Kisumu All Stars (Thika Stadium)

Shabana 3-1 FC Talanta (Gusii Stadium)

Eldoret Youth 2-4 Nairobi Stima (Eldoret Show Grounds)

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends