Wazito FC walenga ushindi wa pili msimu huu

Ligi kuu ya Premier nchini Kenya inaingia wiki ya nane huku mechi sita zikiratibiwa kupigwa kuanzia Jumamosi ambapo wazito FC itakuwa ikilenga kupata ushindi wa pili msimu huu kwa kupimana nguvu Sony Sugar  nayo Tusker itakabiliana  Nzoia Sugar. Chemelil Sugar itapata kibarua dhidi ya Kisumu All Stars.

Siku ya Jumapili  nambari mbili AFC Leopards  itazichapa dhidi ya Ulinzi Stars ,Kariobangi Sharks itakata maungo dhidi ya  Zoo Kericho ilhali Kakamega Homeboyz itazima hasira kwa kukabana koo na  Sofapaka.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends