Wazito FC wamtimua kocha Melo baada ya mechi nne tu

Wazito FC wamemtimua kocha Melis Medo baada ya kuwa usukani kwa mechi nne tu, tangu alipochukua mikoba ya uongozi wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Kandanda Kenya – KPL.

Mmarekani huyo ambaye aliwahi kuzifundisha Sofapaka na Mount Kenya United alichukua nafasi ya kocha aliyepigwa kalamu Ambani mwezi uliopita na akashinda mechi moja pekee, akapoteza mbili na kutoka sare moja. Medo inadaiwa alikuwa na mahusiano mabaya na wachezaji baada ya kuwashambulia hadharani kutokana na matokeo mabaya. Mechi ya mwisho kwa kocha huyo ilikuwa Jumatano wakati walipigwa mabao mawili kwa sifuri na Kisumu All Stars mjini Kisumu

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends