Werner afunga goli baada ya dakika 1,000 Chelsea ikishinda 2-0 kwa Newcastle United na kuingia nne bora

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Timo Werner hatimaye amemaliza ukame wa magoli ndani ya uzi wa The Blues, Chelsea baada ya kutumia dakika 1000 kufunga bao lake akihitaji mechi 14 ili kuisaidia timu yake kuondoka na alama tatu muhimu mbele ya Newcastle United kwa ushindi wa 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la Stamford Bridge Leo Jumatatu.

Werner mbali na kufunga pia alitangulia kusaidia upatikanaji wa bao la kwanza kwa The Blues goli ambalo likiwekwa kimiani na mshambuliaji wa Ufaransa Oliver Giroud ambaye alichukua nafasi ya Tammy Abraham.

Ushindi huo unaifanya Chelsea kukwea mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya EPL juu ya West Ham United.

Wagonga Nyundo wa London walifanikiwa kushinda mechi yao dhidi ya Sheffield United mapema leo Jumatatu 3-0 na sasa wametoshana alama na Chelsea ingawa zote zinakaa chini ya bingwa mtetezi Liverpool.

Mara ya mwisho kufunga goli ilikuwa Novemba 7, 2020.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares