Werner awasha moto wa kufamia nyavu Bundesliga, Leipzig yaichapa Cologne 4-2

Pengine jina hili halitajwi sana kwa sababu ya uwepo wa majina makubwa kinywani mwa wachambuzi na wadau wengi wa Bundesliga kama Robert Lewandowski, Thomas Mulller, Jodan Sancho na mengine lakini Timo Werner ni habari nyingine msimu huu.

Akiifungia timu yake goli la 25 la msimu huu na kuisaidia timu ya RB Leipzig kupata ushindi dhidi ya Cologne wa goli 4-2 na kuendeleza mbio ya kuwania nafasi ya pili dhidi ya Borrusia Dortmund.

Katika mapungufu madogo sana ya walinzi wa Cologne yalipelekea mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani kupachika goli kunako dakika ya 50, ambapo amekuwa mchezaji wa tano kufikisha goli 15 katika viwanja vya ugenini kwa msimu.

Leipzig wanasalia nyuma ya pointi mbili dhidi ya Dortmund huku mechi tano pekee zikiwa zimesalia.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends