Wijnaldum aikacha Barcelona, mbioni kutua PSG

Kiungo mkabaji wa Uholanzi Georginio Wijnaldum amepanga kujiunga na Paris St-Germain kama mchezaji huru baada ya kandarasi yake kumalizika klabuni Liverpool.

Wijnaldum aliamua kutoongeza mkataba mpya ndani ya Liverpool mwishoni mwa msimu na kukaibuka tetesi kuwa anaelekea kumwaga wino ndani ya Fc Barcelona ingawa mambo yamekuwa tofauti kwa sasa.

Wijnaldum mwenye umri wa miaka 30, anaelekea PSG kwa lengo la kuongeza nguvu kwa Mabingwa hao wa Ligi Kuu Ufaransa msimu wa mwaka 2019/20

Uwepo wa kocha Mauricio Pochettino inatajwa kuwa moja ya sababu za kukubali kwenda PSG.

Wijnaldum, ni sehemu ya kikosi cha Uholanzi ambacho kiko kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2020.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares