Wijnaldum, Depay waipa ushindi Uholanzi mbele ya Bosnia

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum ameipa alama tatu timu yake ya taifa kwa kufunga goli mbili katika ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Bosnia-Herzegovina mchezo wa Ligi ya Mataifa barani Ulaya hatua ya makundi uliopigwa Novemba 16. Unakuwa ushindi wa pili kwa Uholanzi katika mechi tano za ligi hiyo ya mataifa.

Wijnaldum alitupia bao la kwanza kwenye dakika sita tu kabla kufunga goli linguine akitumia vyema mpira wa winga wa Tottenham Steven Berghuis kuandikisha goli la kwanza baadae fowadi wa Lyon Memphis Depay akafanya 3-0.

Strika wa Bosnia-Herzegovina Smail Prevljak alipata goli la kufutia machozi ingawa halikutosha kufanya mapinduzi ya matokeo kutokana na ubora aliokuwa nao Uholanzi katika mchezo wa jana.

Katika mchezo mwingine wa kundi A1, Italia walishinda goli 2-0 dhidi ya Poland, matokeo yanayowafanya kuwa juu kwa pointi moja dhidi ya Uholanzi katika msimamo wa kundi hilo.

Author: Asifiwe Mbembela