Wilder hana mpango wa kustaafu licha ya kipigo cha Fury

360

Licha ya kupokea kipigo kizito Bondia Deontay Wilder kikiwa ni cha pili kutoka kwa Tyson Fury amesema hana mpango ya kuachana na mchezo huo.

Maneno hayo yamesemwa na Mwalimu wa Wilder, Bwana Malik Scott raia wa Marekani ikiwa ni siku moja tangia bondia huyo achapwe katika uringo na Fury.

Wilder, 35, juzi alipingwa na Fury katika raundi ya 11 na kupoteza nafasi ya kushinda ubingwa wa dunia wa WBC mtanange uliopigwa Jiji la Las Vegas Marekani.

“Deontay anapigana kwa sababu anaupenda mchezo, lakini tayari familia yake inaishi vizuri kiuchumi, hivyo hapigani kupata fedha”, alisema Scott.

“Ingawa yuko vizuri kiuchumi, kustaafu sio mpango wake kwa sasa, hatujawai hata kujadili”.

Wilder na Fury wamekuwa kwenye ushindani wa maneno mpaka kwenye mataji kwa muda sasa, itakumbukwa Disemba 2018 katika pambano la wawili hao liliisha kwa sare kabla ya kuhitajiana tena na kurudiana Februari 2020 ambapo kocha wa Wilder, Mark Breland alirusha taulo katika uringo wakati raundi ya saba inaendelea ikiwa ni ishara ya kushindwa.

Ingawa baadaye Wilder alikiri kutopenda alichofanya kocha wake Breland kitendo ambacho kilipelekea kumfuta kazi na kumpatia Scott.

Author: Asifiwe Mbembela