Willian awaomba radhi mashabiki wa Arsenal

Winga wa kimataifa wa Brazil Willian amewaomba radhi mashabiki wa klabu ya Arsenal kufuatia kiwango kibovu katika kipindi cha miaka miwili ambacho ametumika klabuni hapo.

Mkataba wa Willian umesitishwa kwa Washika Mtutu wa London ambapo sasa anajiunga na klabu yake ya zamani ya Corinthians ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Brazil.

“Katika kipindi changu chote cha taaluma yangu nimekuwa nikifanya kazi kwa juhudi na bidii kubwa, lakini hapa nimeshindwa. Alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 kwenye ukurasa wake wa Instagram.

“Ubora niliokuwa nao ghafla haujaonekana hapa”.

Willian alijiunga na Arsenal mwezi Agosti 2020 baada ya kuondoka Chelsea kama mchezaji huru ambapo kwa wiki alikuwa analipwa pauni 200,000.

“Nimepokea ukosoaji mkubwa, hata ndani ya klabu wengine wakisema nimekuja kwa sababu za kuvuna pesa, nadhani kusema haya watajua walikuwa wanafanya vibaya”.

Willian – ni mshindi wa Ligi Kuu England mara mbili katika kipindi cha miaka saba The Blues anaenda kujiunga na Corinthians, ambayo alianzia taaluma yake kabla ya kutua Shakhtar Donetsk mwaka 2007.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares