Willian mchezaji wa karibuni kukumbwa na ubaguzi wa rangi

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na sasa Arsenal Willian ameweka wazi kuwa alitumiwa maneno ya kibaguzi kupitia mitandao ya kijamii (Instagram).

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32, raia wa Brazil alipiga picha ujumbe huo na kuusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

“Hatuwezi kuruhusu na hatuwezi kuacha maneno au vitendo vya kibaguzi kuendelea katika jamii ya wapenda soka” ilisema taarifa ya klabu ya Arsenal.

Siku za karibuni kumeibuka vitendo na viashiria vya ubaguzi wa rangi ambapo mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, Marcus Rashford, E walikutana na kadhia hiyo, nyota wa Arsenal Eddie Nketiah pia alikutana na changamoto hiyo.

Bado tiba haijapatikana ya kukomesha tabia kama hizo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares