Wolves yampata Bruno, mrithi wa Nuno Espirito Santo

Klabu ya Wolves inayoshiriki Ligi Kuu England imemtangaza aliyewai kuwa kocha wa Benfica Bruno Lage kuwa kocha wao akirithi mikoba ya Nuno Espirito Santo aliyebwaga manyanga mwishoni mwa msimu uliopita.
Lage alikuwa kocha msaidizi wa Carlos Carvalhal katika klabu ya Sheffield Wednesday na Swansea kabla ya kujiunga na Benfica, ambapo alienda kushinda taji la Ureno mwaka 2019.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45, akizungumza kufuatia kumwaga wino ndani ya vijana hao ambao walifanya vyema chini ya Nuno amesema “Nifuraha kuwa sehemu ya familia hii, natazama katika njia chanya zaidi”.
Lage alikuwa bila kazi tangia kuachia mwezi Juni baada ya kukaa klabuni hapo miezi 18 tu.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares