Xavi kutua Barcelona kama kocha mpya

33

Kwa mjibu wa Mwandishi mmoja wa habari wa Hispania amethibitisha kuwa licha ya kuwa Rais wa klabu ya Fc Barcelona Juan Laporta hajasema nani atakuwa kocha mrithi wa Ronald Koeman, lakini kocha ajaye ni kiungo nguli Xavi Hernandez.

Moja ya sababu ambayo inatajwa kuwa rahisi kufikia makubaliano na Xavi ni mdodoro wa uchumi ndani ya Barca, kinachofanyika ni kuwa na subira pamoja na imani.
Historia ni moja ya sababu pia, itakumbukwa Rais Laporta ndiye aliyempandisha kocha Pep Guardiola kutoka timu ya Barcelona B miaka 13 iliyopita.
Mpaka karibuni kocha Xavi, amekuwa akikinoa kikosi cha Al Sadd kutokea Qatar, na Laporta amefanya mazungumzo mara kadhaa, huku mazungumzo yakiwa kwenye mlengo chanya.
Swali kubwa kwa sasa siyo nani atakuwa kocha mkuu wa Barcelona bali swali ni je, Xavi anaweza kuwa suluhu ya Barca?

Author: Bruce Amani