Yanga mambo safi, Msolla apokea muundo wa mabadiliko

Kamati ya Katiba na Kamati ya Mabadiliko imekamilisha ripoti ya muundo pendekezwa na kukabidhi kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga inayoongozwa na mwenyekiti wa klabu Dkt Mshindo Msolla.

Akikabidhiwa ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Mabadiliko Alex Mgongolwa, Mwenyekiti wa klabu amesema ni hatua nzuri ikiwa kama sehemu ya awali ya mabadiliko, kuwa mfumo huo pendekezwa wa mabadiliko ya uendeshaji wa Yanga umekamilika rasmi na hivi sasa wanakwenda katika hatua nyingine.

Msolla ameongeza kuwa kilichobakia hivi sasa ni kufuata muongozo na baraka kutoka kwa washika dau wa michezo ambao ni wizara yenye dhamana na michezo, Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Fair Competition Commission (FCC), TFF na Bodi ya Ligi Kuu Bara.

Itakumbukwa wakati anaingia madarakani dkt Msolla moja ya ahadi zake ilikuwa ni kuipeleka timu hiyo katika mfumo wa mabadiliko utakaoifanya timu hiyo kujiendesha yenyewe bila kutegemea fedha za wahisani.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares