Yanga, Mtibwa Sugar usipime mchezo wa VPL, Saido Ntibazonkiza ampa “PRESHA” Kaze

Mabingwa wa kihistoria wa VPL klabu ya Yanga ambayo pia ni kinara wa Ligi Kuu nchini Tanzania inashuka dimbani leo Jumamosi kucheza mechi dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo ambao ni ngumu kwa Timu ya Wananchi ambayo inawakosa nyota kibao.

Inashuka uwanjani ikiwa inakumbuka kwamba imetoka kulazimisha sare ya mabao 3-3 na Kagera Sugar kabla ya hapo ililazimisha sare ya 1-1 na Wanakomakumwanya Mbeya City.

Walipokutana mara ya kwanza Uwanja wa Jamhuri, Moro, Yanga ilisepa na pointi tatu mazima kwa ushindi wa bao 1-0 leo inakutana nao Uwanja wa Mkapa.

Nyota watano wa Yanga wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo:- Saido Ntibanzokiza, yeye anasumbuliwa na majeraha ya nyonga aliyapata kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kisha akajitonesha kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba, fainali visiwani Zanzibar.

Beki, Dickson Job majeraha ya nyama za paja yanamsumbua ila ameanza mazoezi mepesi kurejea kwenye ubora wake.

Yacouba Songne taratibu ameanza kurejea kwenye ubora wake baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi, dhidhi ya Azam FC.

Mapinduzi Balama, nyota huyu kwa sasa jezi yake namba 7 ipo mikononi mwa Fiston Abdoul Razack kwa kuwa anatibu majeraha yake ya mguu.

Ramadhan Kabwili, kipa namba tatu wa Yanga hayupo kwenye hesabu za Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Presha kwa Kaze kwa sababu anazidi kupoteza pointi wakati wapinzani wao (Simba) wanazidi kuwasogelea kileleni.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares